11 Januari 2013 - 20:30

jeshi la wanamaji la Urusi linaendelea kufanya mazoezi yake katika eneo la maji ya Siria

wizara ya ulinzi ua Urusi imeeleza kuwa mazoezi hayo yanalenga kuonyesha maandalizi na uwezo wa Urusi katika kutekeleza azma yake ya kulinda mipaka yake,zoezi hili litakusanya kamandi za makomando wa maji pia litatumia anuai za zana za kisasa za kiulinzi.ni muhimu kuashiria kuwa Urusi imetoa uamuzi huo mara tu baada ya kuona majeshi ya Marekani na waitifaki wake yakisogea katika eneo la mashariki ya kati na kuweka kinga za makombora katika mipaka ya Uturuki kwa madai ya kujilinda dhidi ya hujuma za makombora ya Iran na Siria.